Zitto Kabwe: "Hili ni jambo la hatari, kama Serikali isipofanya marekebisho wabunge tusipitishe sheria hii - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 1 February 2018

Zitto Kabwe: "Hili ni jambo la hatari, kama Serikali isipofanya marekebisho wabunge tusipitishe sheria hii

Mbunge wa jimbo la Kigoma , Zitto Kabwe amefunguka na kusema jambo ambalo Serikali inataka kufanya kuhusu fao la matibabu litapelekea watu zaidi ya laki sita katika mfuko wa NSSF kukosa fao hilo jambo ambalo litaongeza shida kwa watumishi. 

Zitto Kabwe amesema hayo jana Januari 31, 2018 wakati akichangia Bungeni juu ya mswada wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa watumishi wa sekta ya Umma na kuwataka wabunge kutoipitisha sheria hiyo kama Serikali haitaifanyia marekebisho kwani kufanya hivyo ni kuwakosesha haki za kimsingi wanachana zaidi ya laki sita wa NSSF.

"Serikali inafanya marekebisho ya sheria ya NSSF, Sheria ya NSSF inatoa 'Health Insurance Benifit' kwa wanachama wa NSSF lakini sheria hii ambayo serikali inaileta hapa inaondoa 'Health Insurance Benefit' kwa wanachama wa NSSF. Hili ni jambo la hatari, sasa hivi NSSF wanazaidi ya wanachama laki sita kwa hiyo Serikali hii inakwenda kutunga sheria kuwaondoa watu laki sita kwenye takwa la kisheria la Health Insurance" alisema Zitto Kabwe

Mbali na hilo Zitto Kabwe aliweza kutoa ushauri ambao Serikali inaweza kuufuata ili mwisho wa siku wanachama wa NSSF waweze kupata haki yao ya msingi ya matibabu pindi mifuko hiyo itakapounganishwa.

"Serikali inataka 'Health Insurance' zote ziwe zinatolewa na NHIF inaeleweka tunachopaswa kukifanya kwenye sheria ni kuweka provision inayosema kwamba fao hilo la Health Insuarance litatolewa na NHIF kwa NSSF kuchukua ile michango inayolipia Health Insurance na kuipeleka NHIF. Hivyo ukiwa na kadi ya NSSF na mwanachama wa NSSF moja kwa moja unakuwa mwanachama wa NHIF, hii ndiyo njia bora kabisa ambayo Serikali inapaswa kufanya na nawashauru ndugu wabunge kama marekebisho haya hayatafanywa tusiipitishe sheria hii kwa sababu tunakwenda kuwaondoa watu laki sita kutoka kwenye 'Health Insurance'" alisisitiza Zitto Kabwe

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here