1.Kama ni mlevi uliyebobea na unahisi huwezikuacha kwa siku moja, anza kwa kupunguza kiwango cha kunywa, yaani kama unakunywa bia tatu kwa siku, anza kunywa moja, baadae moja kwa siku mbili mpaka utakapozoea kuishi bila pombe.
2.Epuka kuweka kilevi au pombe nyumbani au sehemu ya kazi ili kuepuka majaribu.
3.Usipende kuruka mlo, kula chakula mara 3 mpaka nne (4) kwa siku ili kuupatia mwili virutubisho vyote muhimu.
4.Ondoa dhamira potofu kwamba huwezi kuishi pasipo kunywa pombe. Kumbuka mwili wako umeumbwa kikamilifu kukabili hali zote za Maisha hivyo usihisi kuwa pombe ndio kichocheo chako kila unapotaka kufanya jambo Fulani.
5.Zingatia mlo kamili, na jifunze kula matunda kwa wingi.
6.Anza kufanya mazoezi na upange ratiba hii muda ambao ulikuwa ukitumia kunywa pombe.
7.Kumbuka mambo mabaya ambayo yalikutokea kutokana na pombe katika maisha yako. Hii itakusaidia kutothubutu tena kunywa pombe.
8.Ongeza unywaji wa maji jenga mazoea ya kunywa angalau glasi tano (5) za maji kwa siku.
9.Jenga mazingira ya kujizawadia kutokana na uamuzi wako mzuri wa kutokunywa pombe.
10.Washirikishe ndugu, jamaa na mrafiki wa karibu kuhusu uamuzi wako wa kuacha pombe na pia usijione mjinga kwa wale watakao kucheka.
No comments:
Post a Comment