1.Huhifadhi fedha za dharula kwa ajili ya majanga yoyote yanayoweza kutokea. Na ukipatwa na janga lolote, hukurudisha nyuma na kuanza upya. Pia huna tabia ya kulipa madeni/ bili zako mapema na kusubiri ziwe nyingi na “kukomba” kipato chako chote.
2.Unaishi kwa kuangalia watu wengine wanakuchukuliaje… Si mashindano! Eti tu kwa kuwa rafiki yako mpendwa kanunua Simu ya kisasa sana basi kwanini na wewe usiuze ya kwako ununue kama yake bila kujali uwezo wako ni kiasi gani. Au mimi ni mashuhuli sana sitakiwi kuonekana kwenye daladala/bodaboda ntakodi tax.
3.Unawekeza fedha zako kwenye vitu usivyovijua pengine hujapewa elimu ya kutosha, Au basi tu unafuata Mkumbo.
4.Muoga wa kujaribu Njia zingine Mbadala za kujipatia kipato (kukosa maamuzi magumu) na kujikuta unategemea kipato kwa shughuli ya aina moja ambayo pengine imepitwa na wakati.
5. Huamki mapema na umekuwa mtu wa kuchelewa kila siku na hata ukiamka huifurahii siku yako!
6. Huna Subira, Unahitaji hela nyingi kwa haraka na kudharau hela ndogo. Unaamini kuna njia za mkato kwa ajili ya kupata hela ya haraka na utajiri. HAKUNA NJIA YA MKATO .
7. Umekuwa mtu wa reja reja hufanyi manunuzi ya pamoja na kujikuta unatumia kiasi kikubwa zaidi cha fedha
8. Huna Mipango , Huandiki Chochote na kufikiria kuhusu Leo tu
9. Unatumia fedha zaidi kuliko kipato chako tena kwa mambo yasiyokuwa na umuhimu kama ulevi, starehe nk. Na matokeo yake unaishi kwa Kuangalia Leo tu.
10. Unalaumu wengine Kuliko Kujituma. Muda wako mwingi huishi kwa furaha na kila shida ama tatizo linalokupata, unatafuta mtu wa kumlaumu.
No comments:
Post a Comment