Taasisi ya GSM Foundation Ijumaa hii imekabidhi jumla ya mifuko ya simenti 600 kwa mkuu wa wilaya ya Temeke, Bi Sofia Mjema ikiwa ni mchango wake kwa jamii katika kuhakikisha sekta ya elimu.
Bi Sofia Mjema akipokea mfuko wa simenti
Bi Sofia Mjema akipokea mfuko wa simenti
Akiongea wakati wa kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi Sofia Mjema, pamoja na kuwashukuru GSM Foundation ameuelekeza msaada huo katika ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Mbande, shule ambayo ina idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma nje kutokana na ukosefu wa madarasa.
Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa GSM, Halfan Kiwamba amesema hii ni sehemu tu ta jitihada zao katika kuhakikisha sekta za elimu na afya, hasa kwa kizazi kijacho zinahudumia wananchi katika hali ya ubora.
No comments:
Post a Comment