Mwanamuziki kutoka nchini Burundi, Kidumu, amefunguka kwa kusema kuwa Wakenya wengi wanadhani kwamba yeye ni Mtanzania kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa wakuimba kwa lugha ya Kiswahili.
Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya kazi na Lady Jaydee, ameiambia BBC Ijumaa hii kuwa yeye ni Mburundi lakini kuwa karibu na Watanzania kumemfanya aonekane na yeye ni Mtanzania.
“Tanzania ni nyumbani pia, nilikuwa nikienda Tanzania kila mwisho wa mwezi, hata Wakenya wengi wanadhani mimi ni mtu wa Tanzania, walikujakujua baadae kama mimi ni Mburundi, lakini kwa sababu ya Kiswahili changu bado wanasema mimi ni Mtanzania” alisema Kidumu.
Pia muimbaji huyo alizungumzia mpango mpya wa kufanya kazi na wasanii wa Tanzania.
“Mpango upo kwa sababu nilishauanza, niliimba na Lady Jaydee, niliimba na Msechu wote ni Watanzania, na bado na mpango wa kufanya kolabo zaidi,” alisema Kidumu.
No comments:
Post a Comment