Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Morogoro, Afande Sele amempa pole
rapper mwenzake Nay wa Mitego ikiwa ni siku moja toka Baraza la Sanaa la Taifa
limfungie rapper huyo kwa muda usiojulikana baada ya kukutwa na makosa matatu.
Aidha, rapper huyo ametakiwa kulipa faini ya shilingi
milioni 1 pamoja na kuwaomba msamaha mashabiki wa muziki wake.
Afande ameonyesha kutopendezwa na adhabu hiyo huku
akidai kuna wasanii wengi wanafanya vitendo kama vya Nay wa Mitego lakini
hawachukuliwi hatua.
“Sio jambo lakuchukiza likini linafadhaisha pale
unapojiuliza kwani aadhibiwe yeye tu?,” Afande aliuliza kupitia instagram yake.
Aliongeza, “Mbona kuna wenzake wengi tu walifanya na
wanaendelea kufanya makosa kama yake au zaid lakini hawajachukuliwa hatua kama
yeye?. Ni Siasa, mapenzi, undugu au, pole askari wangu mdogo mpiganaji stadi
yatakwisha tu, tutawasimulia kina Shishi Baby, Snusex na wengine kuwa ‘hainaga
ushemeji’,”

No comments:
Post a Comment