Yamkini mshukiwa huyo wa ugaidi alikuwa amefungiwa korokoroni
baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kujaribu kuwashawishi watu kujiunga na mtandao
wa kigaidi wa Al Shabaab.
Alipelekwa katika kituo cha polisi cha Kapenguria, Kaskazini
Magharibi mwa Kenya.
Awali gazeti la Daily Nation limeripoti kuwa mtu huyo anadaiwa
kuvamia kituo hicho kumnusuru mshukiwa aliyekuwa amekamatwa kwa tuhuma za
ugaidi .
Gazeti hilo linasema huenda maafisa hadi watano wameuawa.
Mkuu wa polisi wa kituo hicho Vitalis Ochido anadaiwa
kujeruhiwa.
Ufyatulianaji
wa risasi bado unaendelea.
Tovuti ya habari ya Capital FM imemnukuu mkuu wa polisi Joseph
Boinnet akisema polisi zaidi wametumwa eneo hilo.
“Mshukiwa wa ugaidi aliyekuwa anazuiliwa alitwaa bunduki na
kuanza kuvyatua risasi," Bw Boinnet amenukuliwa. "Kituo hicho sasa
kimezingirwa na juhudi za kukabiliana naye (mshambuliaji) zinaendelea."

No comments:
Post a Comment