Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Gadner G Habash
amekanusha kumdhalilisha aliyekuwa mke wake Lady Jaydee kupitia video ambayo
ilisambaa katika mitandao ya kijamii miezi michache iliyopita.
Akiongea
na Bongo5 Jumamosi hii, Gadner amesema anaheshimu faragha ya muimbaji huyo wa
wimbo ‘Ndi Ndi Ndi’ na kamwe hawezi kufanya kitendo kama hicho.
“Kusema kweli sitaki kulizungumzia suala la Lady Jaydee,
naheshimu faragha yake,” alisema Gadner. “Ile issue ilikuzwa na mitandao ya
kijamii, na mitandao ya kijamii inajua kutengeneza mambo hata yasiyokuwepo,”
Mtangazaji huyo amesema hana tatizo na mwanadada huyo kwa kuwa
kila mtu alisha ‘move on’ na anaendelea na mambo yake.
Katika video ambayo ilisambaa mitandaoni, Gadner alisikika
akisema “Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15
hivi,” kauli ambayo ilichukuliwa vibaya na watu wengi.

No comments:
Post a Comment