Ameambia kongamano kuu la chama cha Democratic mjini
Philadelphia kwamba mkewe ndiye “mfumaji bora zaidi niliyewahi kukutana naye”.
Kwenye hotuba yenye hisia kali, amemweleza Hillary kama “rafiki
mkubwa” na akasimulia walivyokutana na jinsi anavyojitolea katika utumishi wa
umma.
Saa chache awali, mkewe aliibuka kuwa mwanamke wa kwanza nchini
Marekani kuidhinishwa kuwania urais na chama kikubwa
Bi Clinton alihitimisha shughuli za usiku huo wa Jumanne kwa
ujumbe wa video ambapo alisema: “Siamini kwamba tumefanikiwa kuweka ufa mkubwa
zaidi katika dari hili la kioo”, akirejelea hotuba ya mkewe Rais Barack Obama,
Michelle, siku ya kwanza ya kongamano.
“Na iwapo kuna wasichana wadogo huko ambao hawajalala na
wananitazama, ningependa kuwaambia, huenda nikawa rais wa kwanza mwanamke
Marekani na mmoja wenu anaweza kunifuata.”
Awali, Bi Clinton alisimulia walivyokutana katika Chuo cha
Uanasheria Yale mwaka 1971.
“Nilimuoa rafiki yangu mkubwa,” amesema. “Tumekuwa tukitembea na
kuzungumza na kucheka pamoja tangu wakati huo.”
Bi Clinton alipitisha wajumbe 2,382 wanaohitajika
kutawazwa mgombea baada ya jimbo la South Dakota kutangaza matokeo yake.
Katika juhudi za kuashiria umoja
katika chama, mpinzani wake wakati wa mchujo, Seneta wa Vermont Bernie Sanders
alichukua maikrofoni na kumtangaza Bi Clinton kuwa mgombea mteule kwa kauli
moja, tangazo lililokaribishwa kwa shangwe.
Awali, wakati wa hotuba yake rasmi
Jumatatu, Bw Sanders alikuwa ametangaza: "Hillary Clinton lazima awe rais
ajaye wa Marekani.”
Tangazo la Bw Sanders ni kama
marudio ya kongamano la 2008 ambapo Bi Clinton alimtangaza Bw Obama kuwa
mgombea mteule.
Bi Clinton atakabiliana na mgombea
wa Republican Donald Trump katika uchaguzi mkuu Novemba.
Kura za maoni zinaonesha wawili hao
wanakaribiana sana kwa uuungwaji mkono wa wapiga kura.

No comments:
Post a Comment