Kwa Chidi Benz, Babutale ni mtu mwenye umuhimu wa aina yake na
atamheshimu daima kwasababu meneja huyo wa Diamond ametumia fedha nyingi hadi
sasa kwaajili yake.
“Huwezi amini mpaka sasa hivi ninavyoestimate kwamba
Tale anaweza akawa ametumia kama milioni 45, 50, 60. Sio kuwekeza, vitu ambavyo
vimefanyika tayari, lakini sijasaini wala nini,” alisema Chidi kwenye kipindi
cha The Playlist cha Times FM.
“Tale anachokifanya anaonesha
kwamba ‘nia yangu mimi sio lazima tukabane kwenye suala la hela, nia yangu wewe
uwe sawa, uwe okay, uwe poa.’ Kwahiyo ina maana mimi sijasaini lakini
nachukulia kwamba yeye aone kusaini inawekana nikasaini ukaniletea mkataba wa
miaka miwili but mimi sasa naishi na wewe kabisa,” aliongeza.
Chidi anadai kuwa anamchukulia Tale
kama familia yake.
“Kwasababu hata sasa hivi nakaa
kwake, bado niko kwao so yaani kwahiyo hata ukija mkataba labda aniandikie
miaka 20 kwamba haina maana.”
Tale alimsaidia rapper huyo
kumsaidia kuepukana na uraibu wa madawa ya kulevya ikiwa pamoja na kumpeleka
rehab na baada ya kutoka kuingia studio kurekodi nyimbo mpya. Hivi karibuni
aliachia wimbo wake mpya ‘Chuma’ aliomshirikisha Raymond.

No comments:
Post a Comment