
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama amesema kuwa kufanyika kwa maombolezo ya
kumbukumbu za Mashujaa inawakumbusha watanzania kuwa wazalendo.
Akizungumza wakati wa
maombolezo ya kumbukumbu za Mashujaa sambamba na kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru
katika mnara wa kumbukumbu za Mashujaa, leo usiku katika viwanja wa
Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma, Waziri Mhagama alisema kuwa
kufanyika kwa maombolezo ya Mashujaa mkoani Dodoma ni heshima kwa wananchi wa
Dodoma na watanzania wote kwa ujumla.
“Kufanyika kwa
maombolezo haya inatukumbusha watanzania kuwa wazalendo na kupigania
bila kuchoka, bila kujali makabila yetu na tujifunze kwa Mashujaa hawa
waliopigania uhuru wetu” alisema Waziri Mhagama.
Waziri Mhagama
aliwaomba watanzania kutumia siku ya kumbukumbu ya Mashujaa ambayo
ni Julai 25, kwa namna mbalimbali ikiwemo kufanya maombi ya sala kwa
Mashujaa wote walifariki katika harakati mbalimbali za kupigania uhuru wa Taifa
la Tanzania.
Kwa upande wake, Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimwa Jordani Rugimbana aliishukuru Serikali kwa
uwamuzi wa kuadhimisha kumbukumbu za mwaka huu za Mashujaa mkoani
Dodoma, na kusema kuwa kufanyika kwa tukio hilo la kihistoria linakumbusha
uwajibu wa watanzania na Mkoa wa Dodoma utaienzi heshima hiyo.
Aidha, Mkuu wa Wilaya
ya Dodoma mjini Mheshimiwa Christina Mndeme aliwasha Mwenge wa Uhuru katika
kilele cha mnara wa mashujaa mnano saa 6 kamili usiku ikiwa ni sehemu ya maombolezo
ya kumbukumbu ya Mashujaa.
Mnara wa Mashujaa
uliopo mkoani Dodoma ni kati ya vituo 4 vilivyopo nchi nzima ambavyo vimekuwa
na makaburi ya Mashujaa mbalimbali waliopigania uhuru wa nchi ya Tanzania.
Vituo vingine vipo meneo ya Mtwara, Dar es Salaam na Kagera.
Maadhimisho ya kumbukumbu
za Mashujaa kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kesho julai 25, mkoni Dodoma
ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
atakuwa mgeni rasmi.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Christina
Mndeme akiwasha Mwenge wa uhuru katika mnara wa mashujaa kuelekea Maadhimisho
ya Siku ya Mshujaa, hafla iliyofanyika Saa Sita Kamili usiku ya tarehe 25 julai
2016 Mkoani Dodoma.

Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma Mh. Jordan Rugimbana akiongea na baadhi wa viongozi wa serikali
waliohudhuria tukio hilo la uwashwaji wa Mwenge na kumshukuru Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa kuupa heshima Mkoa wa Dodoma wa kuadhimisha siku ya
mashujaa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea na baadhi wa viongozi wa serikali
waliohudhuria tukio hilo la uwashwaji wa Mwenge na kutoa rai kwa watanzania
kuwa wazalendo na nchi yao bila kujali itikadi ya mtu kama walivyofanya wazee
wetu waliopigania uhuru wa nchi.

Wanajeshi wa Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiimba wimbo wa Taifa mara
baada ya kuwashwa kwa Mwenge kuelekea Maadhimisho
ya Siku ya Mshujaa yatakayofanyika tarehe 25 julai 2016 Mkoani Dodoma.

Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa
Serikali wakishuhudia uwashwaji wa Mwenge.

Mwenge wa
uhuru mara baada ya kuwashwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh. Christina
Mndeme, Tarehe 25 julai 2016 Saa Sita Kamili usiku Mkoani Dodoma.

No comments:
Post a Comment