Mkali wa masauti
Christian Bella ameendelea kuonyesha ukongwe wake katika show ya ‘The Black
Tie’ iliyofanyika Jumamosi hii katika ukumbi wa King Solomon jiji Dar es salaam.
Bella akijazwa madola
Muimbaji huyo mwenye asili Kongo, alionyesha uwezo wake mkubwa
wa kuimba hali ambayo iliwafanya mashabiki ambao walijitokeza katika show hiyo
kutoa pesa zao mfukoni na kumtuza msanii huyo.
Akiwa
mwenye furaha jukwaani, Bella alisema pesa ambayo ametuzwa jukwaani kwa usiku
huo zinatosha kumpeleka Afrika Kusini na kushoot video mpya.
“Nashukuru mungu nimepata hela ya video, asanteni sana mashabiki
wangu,” alisema Bella huyu akipiga magoti kumshukuru mungu.
Kwa upande wa muandaaji wa show hiyo, Wema Sepetu kupitia
instagram yake, amempongeza msanii huyo huku akitaja kiwacho cha pesa
alichotuzwa.
“7000$ alitunzwa jana Mzee wa Masauti… Jamani tusubirie Pictures
eeh…. They are coming soo,” aliandika Wema.
Ukiachana na dola hizo, mashabiki wake wengine pamoja na wasanii
wa filamu wakiongozwa na Steve Nyerere, JB pamoja na Irene Uwoya alishindana
kumtuza msanii huyo.
Kiingilio katika show hiyo, kilikuwa ni tsh 50,000 kwa viti vya
kawaida huku VIP iliwa tsh 100,000 na milioni 1 kwa meza nzima.

No comments:
Post a Comment