Wanawake waislamu nchini Rwanda,wapigwa marufuku wasijifunike
nyuso zao.
Hatua hiii imechukuliwa na jumuiya ya waislamu nchini humo
iliyofikia uamuzi wa kuipiga marufuku vazi hilo la Niqab linalovaliwa na
wanawake.
Vazi hilo hufunika uso wote wa mwanamke.
Jumuiya hiyo imesema marufuku hiyo inatokana na sababu za
kiusalama kwa waislamu na vilevile warwandaa Islamic State
'' Hili vazi ni la kiislamu hata hivyo limeanza kutumika vibaya
kwa madhumuni ya kudhuru usalama wa waisilamu na vitendo vinavyokinzana na
mafunzi ya dini ya Kiislamu''
''Jambo la pili ni usalama wa nchi. kwa sababu watu wanajificha
na kutenda vitendo pasi na kutaka kuonekana''.
''Tumeona fikira potofu tayari ikifuja na ndiposa tukachukua
uamuzi huu kuzuia kuenea kwa uovu'' alisema sheikh Mussa Sindayigaya.
Uamuzi huo umetokea wakati kundi la watu 17 wa kiislam
wanazuiliwa nchini humo kwa tuhuma za kutaka kujiunga na kundi la IS na
kufundisha itikadi za kundi hilo.
Katika msikiti mkuu wa Nyamirambo jijini Kigali ni wakati wa
swala ya adhuhuri,,,waislam wengi wanaingia msikitini …lakini huwezi kuona hata
mmoja anayevaa niqab miongoni mwa wanawake au mabinti wanaoingia hapa msikitini
Wanawoiunga mkono kauli hiyo ya jumuiya ya waislam nchini Rwanda
wanasema kuwa Niqab ilikuwa imeanza kutumika kuficha maoavu mengi katika jamii.
Aidha wanasema kuwa wanawake waislamu wanapaswa kuwajibika kwa
kujiepusha na maovu ambayo sasa yameanza kuchipuka kwa kisingizio cha Niqab.
Kuna wengine walioghadhabishwa na uamuzi huo lakini hawakutaka
kuzungumzia suala hilo wakisema wanahofia usalama wao.
Hapo nyuma kundi la waislam zaidi ya 17 lilishikwa na
kufunguliwa mashtaka ya kusajili vijana wa kujiunga na kundi la Islamic State
na pia kueneza itikadi za kundi hilo.

No comments:
Post a Comment