WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick
Sumaye, amekubali ombi la viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Kanda ya Pwani, waliomchukulia fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti
wa chama hicho kanda hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Baadhi ya viongozi hao
waliojitokeza kumchukulia fomu Sumaye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dar es
Salaam, ambaye pia ni Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, Mwenyekiti wa chama
hicho Ilala, Dk. Makongoro Mahanga na Mwenyekiti wa mkoa wa Pwani, Baraka
Mwago.
Baada ya kuchukua fomu hiyo katika
ofisi za Chadema Kanda Kinondoni jana, viongozi hao walielekea nyumbani kwa
Sumaye maeneo ya Tondoroni Kiluvya, mkoa wa Pwani, kwa ajili ya kumkabidhi.
Baada ya kupokea fomu hizo, Sumaye
alikubali ombi hilo na kuzijaza na kuahidi kurejesha leo katika ofisi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari
kijijini kwake mara baada ya kukabidhiwa fomu hizo na Waitara, Sumaye alisema
ni wakati sasa wa kukipeleka chama hicho hadi vitongojini.
Waziri Mkuu huyo mstaafu alihamia
upinzania mwaka jana katika harakati za uchaguzi mkuu akitokea Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na hivi karibuni aliteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema.

No comments:
Post a Comment