Historia za wasanii wengi waliofanikiwa zina mambo mengi
ya kusisimua.
Wengi wamepitia vikwazo vingi lakini ni wale
waliovumilia tu ndio ambao hadi leo wapo na wamefanikiwa sana. Rich Mavoko
ameshare kwa ufupi yale aliyopita kwenye safari yake ya muziki na kutoa ushauri
muhimu kwa wasanii wachanga wanaohangaika sasa.
Akiweka wimbo wake wa kwanza kwa
kuufanyia video, Mavoko aliandika:
Huu ndo ulikuwa mwanzo wangu mwaka 2010 nilitoa hii kazi
ilikuwa ina vikwazo vingi sana ila tukafanikisha locaction kuzingua kwa msanii
uliyefanya nae kazi kutompata kwa muda unaotakiwa ila tulimaliza Mtu ambaye
alifanyikisha hii kazi ni rafiki yangu Rama na Mwenzake Hk haikuwa rahisi
kabisa kama tunavyoiona na mpaka kumpata model pia ilikuwa swala jingine sababu
nilikuwa natamani kufanya nae kazi kwa wakati huo nae alikuwa wa moto sana lulu
ila tukafanikisha ila usichokijua kwenye hii video ndoto yangu kubwa nilitaka
kufanya na Adam juma swala lilikuwa gumu kwa kipindi icho kipato kilikuwa
kidogo ikabidi adam atupe mejja ambae alikuwa visual lab hapo hapo tukashukuru
ila mimi moyo wangu nilitamani sana Adamu juma ndo ilikuwa ndoto yangu kubwa
kufanya nae kazi..
Sikuchoka kujitaidi hatimae video yangu ya silali
nikafanya na alAdam juma pia ni kazi ilikuwa ina matatizo mengi ambayo
kiubinadam sipaswi ya sema namshukuru sana Adam alilimaliza swala ili likiwa
limekaa sawa… rehemvisulab pia siwez msahau alichangia mengi kwenye safari
yangu ya kufanya harakati za kushoot ili nifunzo kwa vijana ambao wanatamani
kuwa wasanii wa mziki huu una vikwazo usije ukawa mtu wa kulalamika mana
kumbuka ivi vitu aviji kirahisi kudharaulika ni kawaida sana tena usije ukasusa
mana haitokusaidia kaza mana safari yake kuna mawili kupata au kukosa ila
moyoni mwako jiekee kupata ili uwe na moyo ata pale unapokesea kwamba ufanye
kwa bidii ipo siku kuchoka kwenye kazii hii ni mwiko pia ni kazi ambayo
inahitaji uwe mpole sana mana kila mtu atatamani kukuelezea tofauti mara
unaringa pale unapo onekana unapata so ishi nao vizuri jaribu ata kujishusha
ishi kama bwege na kuheshim ata kitu kidogo ambacho unaambiwa ingawa mda
mwingine unaona kabisa ichi sio ila sikiliza mana kwenye maneno kumi
utakayoambiwa uwenda kuna ukweli ata robo au nusu.
Hivi karibuni Mavoko alisainishwa
na label ya WCB na kuachia wimbo wake, Ibaki Story

No comments:
Post a Comment