Makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, Dk John Malecela
amemsihi Rais John Magufuli kuendelea na kasi yake na kutaka asibadilike hata
kama akipewa uenyekiti wa chama hicho.
Alisema hayo wakati akizungumza kwa muda mfupi na
waandishi wa habari wakati akikabidhi madawati 127 aliyochangia na marafiki
zake kwa mkuu wa wilaya ya Chamwino, Dodoma.
Dk Malecela aliyewahi kuwa waziri
mkuu na makamu wa kwanza wa Rais, alisema kasi ya Rais Magufuli isiishie katika
serikali tu, bali iingie hadi katika chama.
“Nakubaliana na utaratibu mzima wa
kumkabidhi kijiti Rais Magufuli, lakini nataka akiingia aendeleze kasi hiyo ili
amulike na kuwaondoa wasiofaa kwenye chama”, alisema.
Baada ya kusema hayo alisema
anaiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa kutaka kuhakikisha kila mwanafunzi
anaketi kwenye dawati na kuwaasa walimu kuangalia utunzaji wa madawati hayo.
BY: EMMY MWAIPOPO
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment