
Katibu Mkuu Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Dkt Vicent Mashinji amewataka vijana wa Bavicha kutokuwa wazembe
wakufikiria bali kujipanga kwa ajili ya kushika dola mwaka wa uchaguzi mkuu
2020 huku akiwapatia kanuni za kushinda uchaguzi huo.
Akizungumza na vijana hao jana jijini
Dar es salaam Mashinji aliwaambia vijana hao chama chao kimejipanga kushika
dola hivyo wao kama vijana wanatakiwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya
kufanya uchaguzi na kuwatambua wanachama hai, pia kuhakikisha kuwa uchaguzi wa
serikali za mitaa vijana wanashiriki nafasi mbali mbali na kushinda
”Nataka niwape majukumu matatu
ambayo mkiyafanya hayo 2020 tutashinda nakutangazwa, moja hakikisheni
tunaingiza wanachama wapya na kuwahakiki walio hai, nendeni 2019 kwenye serikali
za mitaa vijana mgombee na tupate viongozi ngazi ya chini viijana wasomi, na
tatu kwa mwaka huu kila kijana ajue nafasi zitakozogombewa katika eneo lake
hiyo itatusaidia kushinda nafasi nyingi za madiwani kwa Tanzania bara na
visiwani na haya ndiyo majukumu makubwa ninayowapatia”
Alisema Mashinji.
Pamoja na hayo aliwataka vijana hao
kuendelea kupigania haki za wanyonge na kushinda vita ya demokrasia bila
kuvunja sheria huku akiwaasa kuwa askari mzuri na shujaa ni yule anayepambana
bila risasi.
”Askari mzuri ni yule ashindaye
vita bila kutumia risasi zake, mkawe mabalozi wa kuwatetea wanyonge na haki
zao, msiwe waoga kudai katiba ya wananchi, pia kuna watu Geita, Shinyanga na
Simiyu tunataarifa wanapigwa kisa itikadi ya upinzani wa vyama hivyo kama
vijana mnatakiwa mpaze sauti kwa ajili yao”. aliwaambia Mashinji.
Hata hivyo Mashinji aliwaasa vijana
hao kuwa wapole na kusubiri maamuzi ya viongozi wa chama kwani yanabusara. Aidha
aliwapongeza vijana hao kwa kuwa na umoja wa kupigania haki na misingi ya
demokrasia.
Mwenyekiti wa Bavicha Taifa
Patrobas Katambi alimweleza Katibu huyo wa chama kuwa wao wapo tayari kwa
pambano japo wanasikiliza na kutii kauli ya chama hivyo wao watatoa
msimamo wao.
”Sisi vijana tupo tayari miili yetu
ilale makaburini na tukumbukwe kama mashujaa waliokufa wakipigania haki,
tumesikiliza maagizo ya viongozi wetu lakini pia sisi leo tutatoa
msimamo wetu”.- Katambi

No comments:
Post a Comment