Mtu huyo anadaiwa kuvamia kituo hicho kumnusuru mshukiwa
aliyekuwa amekamatwa akishukiwa kuhusika katika ugaidi, gazeti la Daily Nation
limeripoti.
Gazeti hilo linasema huenda maafisa hadi watano wameuawa.
Mkuu wa polisi wa kituo hicho Vitalis Ochido anadaiwa
kujeruhiwa.
Ufyatulianaji
wa risasi bado unaendelea.
Tovuti ya habari ya Capital FM imemnukuu mkuu wa polisi Joseph
Boinnet akisema polisi zaidi wametumwa eneo hilo.
“Mshukiwa wa ugaidi aliyekuwa anazuiliwa alitwaa bunduki na
kuanza kuvyatua risasi," Bw Boinnet amenukuliwa. "Kituo hicho sasa
kimezingirwa na juhudi za kukabiliana naye (mshambuliaji) zinaendelea."

No comments:
Post a Comment