Klabu ya NFL, Dallas Cowboys, ndiyo inayoongoza thamani yake
ikiwa $4bn (£3.03bn), na ni mara ya kwanza kwa klabu ambayo haichezi kandanda kuongoza
katika orodha hiyo tangu kuanzishwa kwake 2011.
United, walioongoza orodha hiyo 2011 na 2012, wana thamani ya
$3.32bn (£2.52bn).
Real Madrid ni wa pili kwa $3.65bn (£2.77bn) na Barcelona wa
tatu $3.55bn (£2.69bn).
United, klabu pekee ya Uingereza katika orodha hiyo, walisaidiwa
sana na mkataba wao wa £750m na Adidas, jambo lililoongeza thamani yao licha ya
kushindwa kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Hata hivyo, Manchester United, ndio wenye deni kubwa zaidi
miongoni mwa klabu zilizo katika 25 bora.
Arsenal (23), Manchester City (28), Chelsea (36) na Liverpool
(41) ndizo klabu hizo nyingine za Uingereza zilizofanikiwa kuwa kwenye orodha
hiyo.

No comments:
Post a Comment