
Msafara wa waziri wa sheria na
katiba Dr. Harrison Mwakyembe jana ulipata ajali baada ya gari lililokua
limembeba Mkurugenzi wa mashtaka na makosa ya jinai DPP Biswalo Mganga
kupinduka katika kata ya Bwanga wilayani Chato wakitokea mkoani Geita.
Imedaiwa chanzo cha ajali hiyo ni
dereva kujaribu kuwakwepa watoto wawili waliokuwa wakikatiza barabara ghafla,
taarifa zinadai kuwa katika ajali hiyo hakuna vifo wala majeruhi.



No comments:
Post a Comment