Wafanyakazi wengi kusini mwa India leo wamepewa likizo kwa
sababu ya filamu ya mwigizaji filamu inayoanza kuonyeshwa kwenye kumbi za
sinema leo.Filamu hiyo ni ya mwigizaji nyota wa asili ya Tamil, Rajinikanth.
Hatua hiyo imechukuliwa kuzuia watu kutumia visingizio kama vile
kwamba wanaugua ili wasifike kazini.
Inahofiwa wengine huenda hata wangezima simu zao au kutofika
kazini bila kueleza sababu.
Filamu hiyo kwa jina Kabali inaonyeshwa katika kumbi 12,000 za
sinema leo.
Rajinikanth, ni mmoja wa waigizaji wanaolipwa pesa nyingi sana
bara Asia na mmoja wa waigizaji mashuhuri zaidi kutoka India.
Hata kabla ya kuzinduliwa, filamu hiyo ya Kabali, ambayo
inaangazia uhalifu wa magenge, imejizolea $30m (£20m) kupitia mauzo ya haki
zake.
Itatolewa pia kwa lugha za Kitelugu, Kihindi na Kimalay.
Katika miji kama vile Chennai na Bangalore, baadhi ya
kampuni zimetangaza Ijumaa kuwa siku ya likizo na hata kuwapa wafanyakazi
tiketi za bure wakatazame filamu hiyo.
Kampuni moja inasema imechukua hatua
hiyo kuzuia watu kufika kwa wingi wakiomba likizo siku ya leo.
, mwenye umri wa miaka 65, ameigiza
katika filamu zaidi ya 170, nyingi katika lugha ya Kitamil.

No comments:
Post a Comment