Kwa mujibu wa waandishi katika jarida la Pediatrics, huo ni ni
usafi dhanio,kwani yatokanayo na baadhi ya wadudu huimarisha mfumo wa kinga ya
mwili.
Unyonyaji wa kidole gumba na ung’ataji wa kucha umeonekana
kuzuia baadhi ya alergy.
Kati ya watu elfu moja wenye umri wa kati ya miaka mitano hadi
thelathini na mbili,walifanyiwa uchunguzi kwa muda nchini New Zealand.
Lakini tabia hii ya unyonyaji vidole na ung’ataji kucha
haisaidii watu wenye pumu au mtu anapopata homa kali.
Uchunguzi uliofanywa na kurekodiwa kwa watoto wenye umri wa kati
ya miaka mitano na kumi na moja na wengine waliofanyiwa vipimo ni wenye umri
kati ya miaka kumi na tatu na thelathini na miwili.
Huku thuluthi moja ya watoto hao ni wanyonyaji wa vidole mara
kwa mara au hung’ata kucha zao na katika vipimo walivyofanyiwa watoto hao
wameonekana kuwa wana kiwango kidogo cha kuathirika kutokana na mazingira hewa
au kula vyakula fulani.
Watoto
wanaoweza kupata matatizo ya kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula
vyakula fulani (alergy) kutokana na vitu kama vumbi kutoka majumbani,manyoya ya
paka au mbwa, lakini watoto wenye kunyonya vidole gumba na kung’ata kucha
walikuwa ni chini ya theluthi moja kuliko watoto wenye tabia hii ya unyonywaji
vidole.
Na tabia hii ya unyonyaji vidole au ung’ataji kucha inaonekana
kuwa kinga mpaka wanapofikia umri wa utu uzima.
" kuwa na paka au mbwa majumbani,ndugu au jamaa wanaofanya
kazi mashambani pia imeonekana kuwa ni sababu kubwa inayosababisha mazingira ya
ukuaji wa magonjwa yanayosababishwa na
kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani.

No comments:
Post a Comment