Mamia ya Watu wameuawa tangu kuzuka
kwa mapigano hayo Alhamisi iliyopita hadi sasa, katika mji mkuu wa nchi hiyo
Juba.
Mapigano hayo ni kati ya vikosi
vinavyomuunga mkono Rais wa nchi hiyo Salva Kiir na yale yanayoongozwa na
Makamu wa Rais Riek Machar.
Viongozi hao wawili hivi karibuni
walisaini makubaliano ya amani ya kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe
yaliyodumu kwa miaka miwili.
Awali Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki-moon amezielezea ghasia hizo zilizoanza tena Sudan kusini, kama
zisizo na sababu na hazikubaliki. Amewataka viongozi hao kuyaagiza majeshi yao
kujiondoa katika mapigano.
Kwa upande wake Mjumbe wa Umoja wa
Mataifa, Sudan kusini Shantal Persaud amesema kambi za pande zote mbili mjini
Juba zimeshambuliwa na silaha nzito. Hali inayotishia mamia ya raia kujikuta
kuwa wakimbizi.
Aidha amewekea matumaini ya
kutekelezwa kwa Makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka uliopita.

No comments:
Post a Comment