Mtangazaji mkongwe nchini, Gadner G Habash, baada ya kurejea tena kwenye
kituo chake cha awali, Clouds FM akitokea EFM, amefunguka na kuzungumzia maisha
yake mapya ndani ya kituo hicho.
Mtangazaji
wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Gadner G Habash
Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii,
Gadner amesema kurudi Clouds FM sehemu ambayo alikaa kwa muda mrefu ni kitu
ambacho kimemfariji sana.
“Maisha ni mazuri sana, ni maisha
kama ukurasa mpya ambao nimeufungua,” alisema Gadner. “Namshukuru sana sana
Mwenyezi Mungu amenipa kipaji lakini nawashukuru zaidi management ya Clouds FM
kuona kwamba ninafaa nirudi pale tushirikiane tena, kwangu mimi naona ni kitu
kikubwa japokuwa nilifanya kazi na Clouds FM kwa miaka 9 lakini bado hii
nimeiona kama ni ukurasa mpya na nikitu kipya na ndio maana unasikia nasound
kama mtu mpya,” alisema Gadner.
Pia mtangazaji huyo alizungumzia
aliwezaje kurudi tena Clouds FM wakati tayari alishaanza maisha mapya na vituo
vingine vya redio kama EFM.
“Ilikuwa ni vigumu sana kuondoka
pale nilipokuwa (EFM) kwa sababu ya mazoea na urafiki ambao tulikuwa nao baina
yangu mimi pamoja na staff ambao nilifanya nao kazi, baina yangu pamoja na
viongozi, lakini wakati mwingine unapofanya uwamuzi, unahitaji kutumia hekima
sana ili ufanye uwamuzi bila kuwa na hisia za kibinafsi, ufanye uwamuzi
kutokana na nini biashara inataka, au ni nini maslahi yanataka na ndo utumie
akili kuona kama maslahi yao. Zaidi ya hapo ujitahidi uondoke kwa mazingira
yalio salama bila kukwazana na wale unaoachana nao, lakini ilikuwa ni ngumu,
lakini kwa sababu Clouds FM walikuwa wananithamini kiukweli wamenipa offer
ambayo ni kubwa sana na unajua wakati mwingine unamuomba mungu, lakini Mungu
anakuletea bila kujua kama anakuletea nafikiri katika dua zangu ambazo
nilimuomba Mungu aniongezee naona mkataba wangu mpya wa Clouds ameniongezea,”

No comments:
Post a Comment