Hali ya utulivu imerejea mjini Juba, Sudan Kusini baada ya Rais
Salva Kiir na Makamu wa Rais Riek Machar kuagiza wanajeshi watiifu kwao
kusitisha vita.
Mji wa Juba umetikiswa na mapigano makali tangu siku ya Ijumaa
ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 300.
Ingawa vita vimesitishwa, maafisa wa utoaji misaada wanasema
hali bado ni mbaya mjini humo na watu wengi hawana vyakula na maji.
Maelfu ya raia walikimbilia makanisani na katika vituo vya Umoja wa
Mataifa kutafuta hifadhi
Rais Kiir na Dkt Machar kwa sasa wanakabiliwa na
shinikizo kutoka kwa Umoja wa Mataifa, Marekani nan chi jirani kuheshimu
mkataba wa Amani ambao walitia saini mwaka jana.
Mkataba huo ulikomesha vita vya
wenyewe kwa wenyewe vilivyokuwa vimezuka Desemba 2013.
Viongozi hao wametakiwa kuhakikisha
taifa hilo halitumbukii tena kwenye mapigano.

No comments:
Post a Comment