Udaili TCU waanza kesho kudahili wanafunzi wa vyuo Vikuu - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 19 July 2016

Udaili TCU waanza kesho kudahili wanafunzi wa vyuo Vikuu

  

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), itaanza kudahili wanafunzi waliomaliza kidato cha sita wanaoomba kujiunga na vyuo vikuu kuanzia kesho. 


Akizungumza jana, Kaimu Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka wa TCU, Dk Kokubelwa Mollel alisema udahili kwa wenye diploma utaanza Julai 31. 

Dk Mollel alisema kazi hiyo itaendelea kwa mwezi mzima ili kuruhusu wananchi wengi zaidi kupata fursa ya kuomba kudahiliwa na udahili huo utafanyika kwa njia ya mtandao.

Alisema ili wanafunzi waweze kuelewa programu zinazotolewa na vyuo vikuu, tume hiyo imeandaa maonyesho ya 11 yatakayofanyika kuanzia Julai 20 hadi 22, mwaka huu. 


Alisema maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here