Obama ameomba uvumilivu utawale
mioyo ya wakaazi wa mji wa Baton Rouge Louisiana nchini Marekani ambao sasa
wanahofu ya kuzuka mashambulizi ya kulipiza kisasi.
Obama aliyasema hayo katika hotuba ya moja kwa moja
kupitia kwa runinga kutoka ikulu ya WhiteHouse muda mchache tu baada ya mtu
mmoja mweusi kuua maafisa watatu wa polisi hukohuko Baton Rouge alikouawa mtu
mweusi
Alton Sterling pasi na hatia yeyote
majuma mawili yaliyopita.
Hasira imekuwa ikitokota miongoni mwa watu weusi baada
ya mtindo wa kuuawa kwa wanaume weusi na polisi wazungu kuendelea kwa muda
mrefu ilihali hakuna hatua inayochukuliwa dhidi yao.
Gavin Long ambaye ni mwanajeshi wa
zamani alikuwa amerekodi ujumbe katika mji wa Dallas siku chache baada ya
polisi watano kuuawa mjini humo katika shambulizi lililotekelezwa kulipiza
kisasi cha mauaji ya Sterling.
Sasa imebainika kuwa Long alikuwa ameweka video kwenye
mtandao akilalamika jinsi polisi wanavyowatendea waamerika weusi ambapo alitoa
wito kwa wanaume weusi kujitolea kuokoa jamii yao.
Long mwenye umri wa miaka 29
aliwahi kuhudumu kama mwanajeshi wa Marekani .
Rais Obama ameshauri watu weusi
dhidi ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya Polisi akisema mauaji ya kulipiza
kisasi sio suluhisho la tatizo sugu la ubaguzi wa rangi bali utachochea uhasama
zaidi dhidi yao na polisoi wazungu.

No comments:
Post a Comment