Rapper Roma Mkatoliki kupitia wimbo wake mpya ‘Kaa Tayari’ amekiibua
kitu kilichopo lakini ambacho hakuna mhusika aliyewahi kukisema hadharani.
Kitu hicho ni meneja wa Tip Top Connection, Babutale
kuwekeza muda wake mwingi zaidi kwa Diamond na label ya WCB kuliko anavyofanya
kwa kambi hiyo ya Manzese.
Kwenye wimbo huo, Roma anasikika akirap: “Bosi kamganda Dangote kaisahau Tip Top.”
Muimbaji na mmoja wa wasanii wa
miaka mingi wa Tip Top, Madee amesema wanautafakari mstari huo kama una ukweli
na watakuja na jibu rasmi.
“Tumeusikia mstari wa @Roma_Mkatoliki na bado tunautafakari km
unaukweli wowote…thn tutawajibu,” Madee
ameandika kwenye Twitter.
Wiki iliyopita Said Fella
aliuelezea mstari huo na kudai kuwa ni jambo ambalo amekuwa akimueleza Tale
kuwa nalo makini.
“Unajua Roma ni mtu mzima,
alichoimba hata mtaani huko watu wanasema, na unaweza kuona labda Roma
ameambiwa hayo maneno na msanii kama Madee au msanii mwingine yeyote wa kwetu.
Lakini hata mimi nilishawahi kumwambia mdogo wangu Babu Tale kuwa tufanye yote
lakini yeye asiisahau Tip Top Connection na mimi nisiisahau TMK,” Fella
alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.
alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.
Hadi sasa ni Madee na Dogo Janja
pekee wamebaki kuwa wasanii wa Tip Top wanaosikika zaidi kuliko wengine. Kundi
hilo limewahi kuwa na wasanii wakali wengine wakiwemo MB Dog, Tundaman, Cassim
Mganga, Keisha, Z-Anto na wengine.

No comments:
Post a Comment