Hivi
karibuni kumekuwepo na tetesi kuwa wasanii wengi waliokuwa wakifanya kazi na
Nahreel wakiwemo Weusi wameikimbia studio yake ya The Industry baada ya
kubadilisha utaratibu wa kurekodi nyimbo.
Jux kwa upande wake amekanusha na kudai kuwa Nahreel bado ni
mshkaji wake mkubwa na mwishoni mwa wiki walikuwa pamoja. Anadai kuwa bado ana
kazi nyingi kwa producer huyo na kwamba wakati mwingine huamua kubadilisha
ladha ili kuogopa nyimbo zake kuzoeleka.
“Nahreel mimi amenitolea hit song, amenitolea ‘Looking For You,
naweza kusema ndio wimbo ambao hata Kiafrika ndio ilifanya poa sana,” Jux
ameimbia Bongo5.
“Hata kuna wasanii wakubwa wa Kiafrika wengine ambao siwezi
kuwasema sasa hivi wameiskia na wameniona huku na tunakuja kufanya nao nyimbo
baadaye, ni sababu ya Looking For You. Nisingetoka kwa Bob labda nisingepata
kitu tofauti,” amesisitiza.
Kingine amedai kuwa muda wote huu hakuwepo alikuwa nchini China
na pia Nahreel amekuwa na miradi yake mingine mingi ikiwemo kwenda Afrika
Kusini kufanya video za Navy Kenzo na za wasanii wa The Industry.
“Karudi, tumekutana jana, bado mshkaji wangu na bado nafanya
naye kazi pia, sababu ya yeye kubadilisha utaratibu wa studio mimi
haijaniathiri chochote kwasababu ni program zake yeye mwenyewe alizotaka
kufanya, kwahiyo mimi naona ni sawa. Kwanza mimi ni mmoja wa watu niliyeona
hivyo yaani Nahreel alikuwa anadeserve hicho kitu pia kwasababu alikuwa
anafanya kazi sana.”
Wiki iliyopita Jux aliachia wimbo wake mpya, Wivu aliorekodi
kwenye studio za AM Records.

No comments:
Post a Comment