
Huyu mke nilimuoa akiwa
hana kitu, kwa bahati alitafutiwa kazi na ndugu yake kwenye kampuni moja ya
simu akawa analipwa kama milioni 3 kwa mwezi fasheni na yeye yeye na fasheni
vipodozi kila aina,handbag na nywele za laki mbili ndio mshahara wake ukawa unaishia
huko mimi mshahara wangu hauzidi laki sita,nilifanyishwa vituko vyote ndani ya
nyumba ,manyanyaso yote ,hapiki hafui,hafanyi chochote ndoa ikawa inaelekea
kuvunjika.
Nikaenda mahakamani kuprocess talaka wakasema
mpaka nianzie baraza la usuluhishi la kata au kanisani,nikaamua kwenda kanisa
tulilofungia ndoa tukaitwa kwa Baba Paroko for hearing sijui mediation sijui
arbitration sijui mie nikatinga kwa bajaj ya kukodi nimepaukaaa yeye akaja na
RAV4 .
Baba Paroko alivyotusikiliza akaaniita pembeni
akasema kijana hapa nadhani hata tukiomba na kukariri mistari yote ya biblia
plus mapambio yote ndoa yako haitarudi kama mwanzo pambana utafute hela ,huyu
ni mchaga katumwa pesa mjini
Nilisali sana nikasugua goti nikamuomba Mungu mara
mambo yangu yakakaa sawa mshahara ukawa mara mbili plus marupurupu anagalau .
baada ya miezi miwili sina hili wala lile mara simu yangu nilishangaa mke wangu
kunipigia mchana ,tumeachishwa kazi kmpuni imeuzwa,hureeeeee niliruka ruka kwa
furaha sana nikapigia simu washikaji tukaenda kunywa bia na nyama choma mpaka
saa sita usiku kabla polisi na makonda hawajatuvamia nilijua ile kazi ndio
inaniharibia ndoa na aliipata kibahati hawezi tena kupata kazi kama ile.
Hela yote ya NSSF akajaribu kufanya kila biashara
biashara zikabuma mtaji ukakata alijifanya hajui kupika sasa anapika kuliko
hata wapishi wa Kempinski,alijifanya sijui hawezi kufua sasa anafua kuliko dobi
,kitandani alijifanya mvivu sasa yuko vizuri kuliko wacheza shoo wa fally ipupa
,RAV4 imepaki tu muda wote ananilelea watoto kwa nini nisimshukuru Mungu
Funzo:
Wanawake Msijisahau sana pale mnapokuwa vizuri
kifedha zaidi ya mume

No comments:
Post a Comment