
Katika majira ya joto, watu husikia hasira au kuwachokoza
wengine mara kwa mara hivyo mioyo yao inaweza kudhurika. Matibabu ya kichina
yanasisitiza kwamba katika majira ya joto, watu wanatakiwa kuzingatia afya ya
moyo wao. Kwa hiyo tutaandaaje maisha yetu kwa ajili ya kujenga afya ya mioyo
yetu?
Kwanza ni kufanya mazoezi ya mwili asubuhi, lakini usifanye mazoezi mara moja baada ya kuamka bali kunywa kikombe kimoja cha maji halafu fanya mazoezi kidogo na lazima ukumbuke kuwa usifanye mazoezi kupita kiasi.
Pili ni kulala kidogo adhuhuri baada ya kula chakula cha mchana, unaweza kuamua kulala wakati wa saa tano hadi saa saba mchana ambao ni wakati unaofaa zaidi kwa kulinda afya ya moyo wako. Aidha kulala kidogo mchana pia kunaweza kukusaidia kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo, na hata kama huwezi kupata usingizi, basi fumba macho yako na kupumzika kidogo.
Tatu ni kunywa chai kidogo alasiri, kwani potassium ndani ya mwili wako inaweza kupotea kirahisi katika majira ya joto, na kunywa chai kunaweza kukusaidia kuhifadhi potassium mwilini.
Nne ni kulowesha miguu yako ndani ya maji ya moto kila usiku na kujikanda au kujichua kidogo mwenyewe ambapo itasaidia mzunguko wa damu mwilini na kusaidia kulala vizuri.

No comments:
Post a Comment