Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian
Lubuva, aliyama hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, baada
ya kutembelea banda la tume hiyo katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya
Kimataifa (Sabasaba), yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Alisema katiba inayopendekezwa
itaweka maoni ya wananchi juu ya mapendekezo ya tume huru ya uchaguzi
wanayoitaka na hivyo uchaguzo ujao utakuwa katika mfumo huo.
Jaji Lubuva alisema ili kufanyika
kwa kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa, ni lazima kwanza Tume ya Taifa ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na NEC zikutane ili kufanya marekebisho ya sheria ya
taifa ya uchaguzi.
"Ni matumaini yetu na
tungependa sana kuona kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu ujao 2020, tuwe
tumeshapata katiba mpya ambayo itatupa muongozo wa uchaguzi mkuu huo," alisema.
Alisema ili kupata tume ya uchaguzi
ambayo itakuwa huru, itatokana na kupatikana kwa katiba mpya ambayo mchakato
wake unatarajiwa kumalizikia kwenye kura ya maoni.
Hata hiuvyo, Jaji Lubuva alisema
tume iliyopo ni huru kwa sababu haiingiliwi na mtu yoyote isipokuwa
kinachosabisha isionekane huru ni mfumo wake wa kuteuliwa kwa makamishna nane
na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama.
"Tume iliyopo ni huru na haki
kwa sababu kazi zetu haziingiliwi na yeyote na hata uchaguzi tulioufanya mwaka
jana ulikuwa huru na haki isipokuwa watu walishaaminishwa tume siyo huru,
" alisema Jaji Lubuva na kuongeza:
“Wanachokitaka Watanzania ni kuona
wanakuwa na tume huru ya maandishi pamoja na isiyoingiliwa na yeyote. Nchi yetu
ina tume huru na haki, ni tofauti na nchi nyingine ambazo zipo kwenye maandishi
tu lakini si huru.”
Juzi Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC,
Ramadhani Kailima alisema uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura
utafanyika mwaka wa fedha wa 2017/18.
Alisema kura ya maoni ya Katiba
inayopendekezwa inaweza kufanyika kabla au baada ya uboreshaji wa daftari hilo.
Hata hivyo, alisema daftari hilo
litaanza kiboreshwa mara baada ya sheria ya uchaguzi kufanyiwa marekebisho na
kupitishwa.

No comments:
Post a Comment