Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald
Trump ameahidi kumaliza uhalifu na ghasia nchini Marekani iwapo atachaguliwa
kuwa rais kwenye uchaguzi mkuu mwezi Novemba.
Akiongea katika kongamano kuu la chama cha Reublican wakati wa
hotuba yake ya kukubali uteuzi, mgombea huyo amesema hakuwezi kuwa na ufanisi
bila kuwepo utawala wa sheria.
Aidha, ameahidi kuchukua hatua kali kukabiliana na wahamiaji
haramu na akaonga kuwa kwa sasa wahamiaji wanaruhusiwa kuingia na kuishi katika
jamii za Marekani bila kuzingatia usalama wa umma.
Bw Trump amejieleza kama mkombozi na sauti ya wanyonge na watu
waliosahaulika nchini Marekani, na akajionyesha kama mtu mwenye sifa tofauti na
mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton ambaye sana amemuonesha
kama mtu mfisadi na asiyewajibika.
Mfanyabiashara huyo tajiri kutoka Marekani amesema atakomesha
sera ya kujenga mataifa na kufanikisha mageuzi ya serikali katika nchi nyingine
ambayo amesema imefeli
Amesema sera hiyo ndiyo chanzo cha matatizo yanayoshuhudiwa
nchini Iraq, Libya, Misri na Syria.
Ameahidi kufanya kazi na washirika wote wa Marekani wanaotaka
kuangamiza kundi la Islamic State.
Ameituhumu Uchina kwa wizi wa haki miliki za Wamarekani,
na kuieleza Beijing kama taifa lililohadaa zaidi katika thamani ya sarafu yake
katika historia.
Bw Trump ameahidi kushauriana upya
na washirika kuhusu mikataba ya kibiashara kuhakikisha Marekani inafaidi.

No comments:
Post a Comment