Utafiti wa kimataifa
umegundua kuwa kunenepa kunahusiana moja kwa moja na visa vya watu kufa mapema,
huku wanaume wakiwa katika uwezekano mara tatu wa kufariki zaidi ya wanawake.
Kwa kutumia data
kutoka takriban watu milioni 4 kutoka mabara manne, Utafiti huo uliochapishwa
katika jarida la Lancet unaashiria kwamba watu wanene wanakufa kwa kiasi cha
miaka mitatu mapema tofauti na watu walio na unene wa kawaida.
Watu walio na unene wa
kupindukia wanapoteza miaka kumi ya maisha yao ambayo wangeweza kuishi.
Wanasayansi wanasema
kwamba kuwa na uzito mkubwa wa mwili kunaongeza hatari ya kuugua maradhi ya
moyo na ya mapafu, kiharusi na saratani.
Utafiti huo mpya
unatofautiana na matokeo ya utafiti wa awali yaliyoashiria kwamba kuwa mnene
kuna manufaa ya kuishi zaidi.
Badala yake watafiti
wanasema moja kati ya vifo vitano vya mapema Marekani na moja kati ya vifo 7
vya mapema Ulaya, vinatokana na kunenepa kupindukia.

No comments:
Post a Comment