
ZITTO Kabwe na Maalim Seif Sharif
Hamad kwa pamoja wameitwa jijini Philadelphia, Marekani.
Maalim Seif ni Katibu Mkuu wa Chama
cha Wananchi (CUF) ambapo Zitto ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo.
Wanasiasa hao wameitwa kuhudhuria
mkutano mkuu wa Chama cha Demokratiki utakaomthibitisha Hillary Clinton kuwa
mgombea urais wa Marekani kupitia chama hicho.
Marekani inatarajia kufanya
Uchaguzi Mkuu tarehe 8 Novemba mwaka huu ambapo Clinton atathibitishwa kwenye
mkutano huo kupambana na Donald Trump wa Chama cha Republican.
Maalim Seif na Zitto ndio wanasiasa
pekee nchini waliopata mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.
Abdallah Khamis, Ofisa Habari wa
ACT- Wazalendo amesema wakati Zitto akiwa kwenye mkutano huo, atapata fursa ya
kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kisiasa duniani.
Taarifa zinaeleza kuwa, viongozi
hao ni wawakilishi wa wanasiasa mahiri kutoka upinzani nchini Tanzania.

No comments:
Post a Comment