Msanii mkongwe wa
muziki na mtangazaji, Soggy Doggy amefunguka kwa kudai kuwa wasanii wake bora
wa muziki wa R&B ni Rama Dee, Nuruelly pamoja na Belle 9 na wengine walio
baki wanaishi kwa promo tu na sio uwezo.
Akiongea katika kipindi cha Enewz kinachoruka katika
runinga ya East Africa Television, Soggy Doggy amesema kukaa kwake kwa P Funky
Majani kama producer msaidizi kumemfanya awatambue wasani ambao hawana vipaji.
“Mimi nashangaa watu wanajipa sana
maflag, mwanamuziki mzuri wa R&B Tanzania nakutajia tatu bora yangu, namba
moja ni Rama Dee, namba mbili ni Nuruhelly na namba tatu ni Belle 9,” alisema
Belle. “Lakini kuna watu wengine wanapewa mipromo, mimi nimekaa studio nimekaa
studio Bongo Record kama producer msaidizi wa P Funk, kwa hiyo mimi namjua mtu
akiimba kwenye key au akitoka, najua sauti ya mtu,”
Aliongeza, “Jamini kuna watu
wanaimba, ukimsikiliza Rama anaimba, ukimsikiliza Nuruelly bad news, lakini
huwezi kumkuta mtu anampa attention kidogo, mtu anasubiri aimbe kama Wanigeria,
so hii imesababisha watu wenye vipaji vyao kufanya mambo mengine,”

No comments:
Post a Comment