
Watu 80 wameripotiwa kufa ikiwa ni
pamoja na watoto 18 katika shambulizi la kigaidi lililotekelezwa jana katika
mji wa Nice nchini Ufaransa.
Tukio hilo limetokea baada ya mtu
mmoja mwenye bunduki aliyekuwa anaendesha Lori kuvamia katika eneo lenye mkusanyiko
wa watu waliokuwa wakisherehekea maadhimisho ya Bastille ambapo mafataki mengi
hurushwa.
Kwamujibu wa The Guardian,
mshambuliaji huyo alirusha risasi kiholela (zigzag) akilenga kuua idadi kubwa
zaidi kadiri awezevyo.
Mwendesha mashtaka katika mji wa Nice, Jean- Michel Pretre, amesema Polisi walifanikiwa kumpiga risasi na kumuua mshambuliaji huyo aliyeendesha Lori lake umbali wa kilometa 2 akitekeleza tukio hilo.
Mwendesha mashtaka katika mji wa Nice, Jean- Michel Pretre, amesema Polisi walifanikiwa kumpiga risasi na kumuua mshambuliaji huyo aliyeendesha Lori lake umbali wa kilometa 2 akitekeleza tukio hilo.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande
amelitaja tukio hilo kuwa baya la kigaidi na kuahidi kuwa nchi yake itakuwa
imara na itapambana na magaidi ndani na nje ya mipaka yake. Alisema tayari
ameamuru jeshi kuingilia kati kuwasaidia polisi hususan katika maeneo ya
mipakani.
Hollande ameitisha mkutano wa
dharura jijini Paris huku hali ya hatari dhidi ya mashambulizi ya kundi la
Kigaidi ya ISIS ikiendelea. Hata hivyo, hadi sasa hakuna kundi lolote
lililobainisha kuhusika na tukio hilo.

No comments:
Post a Comment