
Kiongozi wa Chama Cha ACT
Wazalendo, Zitto Kabwe na katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif
Sharif Hamad wamekutana Katika Mkutano Maalum wa Viongozi wa Kisiasa
Ulimwenguni (International Leaders Forum) ambao umefanyika jana ‘Kwa Saa
za Marekani’ Jijini Philadelphia.
Mkutano huo ulioandaliwa na asasi
ya NDI ‘National Democratic Institute’, ni Sehemu ya matukio maalum kuelekea
Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats (Democratic National Convention), Mkutano
ambao utamthibitisha Bibi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais Kupitia Chama
Hicho.
Zitto Kabwe Pamoja Na Katibu Mkuu
wa CUF, Maalim watakuwa Philadelphia mpaka Siku ya alhamis ambapo mkutano
huo unategemewa kumuidhinisha Bi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais wa Marekani
kupitia Chama Hicho.



No comments:
Post a Comment