Bi Mikaela Kellner na wenzake ambao
pia ni maafisa wa polisi walikuwa wametoka kazini na kufululiza hadi ufukweni
kujitanua chini ya jua.
Mara wakagundua bwana mmoja
aliyekuwa akinadi vitabu vya watoto yatima dakika 15 zilizotangulia alikuwa
amewaibia simu ya mkononi .
Wakashtuka na kuanza kumfuata mbio
ufukweni.
watu waliokuwa wakijivinjari
ufukweni walidhania kuwa mwanamke huyo aliyekuwa nusura uchi alikuwa akifanya
mazoezi kwa jazba ya mwaka.
''Mbona hakuenda rio kwenye
mashindano ya riadha ya olimpiki?
alisikika mama mmoja akimbeza.
Kufumba na kufumbua wakashtuka
binti huyo aliyekuwa amevalia Bikini ''yaani sindiria na chupi'' pekee alikuwa
akikabiliana na mwanaume fulani.
Hapo ndipo walipong'amua haikuwa
mazoezi, na walipopeleleza wakagundua kuwa alikuwa ni afisa polisi aliyekuwa
akimbana mwizi.
Lakini kwasababu huyo mwizi
alijifanya ''dume'' ilimbidi kumbwaga sakafuni kwa mieleka na mateke
mazitomazito.
Waandishi wa habari waliofika
katika bustani hiyo ya Ralambshov baada ya kushuhudia purukushani hiyo
walipigwa na butwaa alipowaeleza kuwa alikuwa ni ''afande'' aliyekuwa kazini
kumnasa mwizi.
Bi Kellner amekuwa maarufu sana
baada ya picha yake akiwa na pikini kuchapishwa katika majarida ya habari
nchini humo.
Chini ya saa 24 baada ya tukio huyo
totoshoo huyo amepokea uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa wenyeji.
Ukurasa wake wa Instagram umepata
ongezeko la zaidi ya wafuasi 9,000 tayari.
No comments:
Post a Comment