
Leo(jana) nimeamua kuchukua uamuzi
wa kutoa agizo kali kabisa toka nimeteuliwa.
Najua litazua maswali, lakini Kwa
kuwa litaokoa maisha ya wanawake wajawazito wa nchi yetu (CEmOC) na wananchi
wengine, nimelitoa. Nitalitetea. Nitalisimamia!
Nimeagiza maDED na maDMO wote nchini
kuhakikisha wana theatres ZENYE KUFANYA KAZI IPASAVYO kwenye vituo vyote vya
Afya kwenye maeneo yao. Wiki iliyopita nilitembelea Manispaa ya Ilala, kwenye
vituo vya afya vitatu nilivyotembelea hakukuwa na theatre yenye kufanya
kazi.
Kwa mujibu wa sera ya afya ya
Tanzania, 'kituo cha afya' kitakuwa na hadhi hiyo kama kina uwezo wa kufanya
upasuaji. Vinginevyo hiyo ni zahanati. Mara nyingi watendaji hawa wamekuwa
wakijificha kwenye kichaka cha 'hatuna fedha', wengine wakiomba fedha kutoka
serikali kuu.
Nilimuuliza Mkurugenzi wa Ilala,
unakusanya sh ngapi Kwa mwezi, akasema bilioni 6. Nikamuuliza unadhani ni sh
ngapi kuwa na theatre yenye kufanya kazi? Akakosa jibu. Nikampa miezi 6 awe na
theatre zenye kufanya upasuaji.
Leo(jana) nimefanya ziara yangu
mikoa ya Shinyanga na Simiyu, nikitimiza mikoa 24. Huku pia nimekutana na
tatizo hilo hilo nilipokuwa Kishapu, Shinyanga na Mwanhuzi, Simiyu. Hawa wa
Meatu wenyewe wana kituo cha Afya Mwandoya, takriban Km 60 kutoka Hospitali ya
Wilaya ya Meatu, pale Mwanhuzi. Wamekipa uwezo wa kufanya upasuaji. Wamenunua
vifaa, wameajiri hadi Daktari (MD) kwa ajira ya muda kwa ajili ya kufanya kazi
pale.
Kituo kimefanya takriban operation
40, zote salama Kwa asilimia 100. Wamepunguza msongamano Mwanhuzi na wamepeleka
huduma nyeti na za kuokoa maisha Karibu zaidi na wananchi, ukizingatia huku
hakuna barabara za lami na hakuna ambulances. I was impressed.
Nikasema sababu za kuwa Halmashauri
hazina pesa huku zinakusanya mamilioni ambayo wanayatumia bila ku-address matatizo
ya msingi ya wananchi hazikubaliki. Leo iwe mwisho. Nimeagiza wakurugenzi wa
Halmashauri zote nchini washirikiane na maDMO wajue watakavyofanya wahakikishe
wanafungua huduma za upasuaji kwenye vituo vyote vya afya nchini ndani ya miezi
sita (6).
Baada ya miezi hiyo sita mimi
mwenyewe na timu yangu ya kurugenzi ya ukaguzi na uhakiki ubora wa huduma za
afya (inspectorate and quality assurance) tutasambaa nchi nzima kukagua huduma
hizi na pale ambapo hatutozikuta tutakishusha hadhi kituo hicho kutoka ngazi ya
'kituo cha afya' na kuwa ngazi ya 'zahanati' sambamba na kuwashauri wenzetu wa
Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuwa wakuu hao wa idara wameshindwa kutekeleza majukumu
yao na hivyo wawashushe vyeo.
Nitasimamia uamuzi huu Kwa nguvu
zangu zote. Sababu ni kwamba ninajua faida yake. Ninajua Mungu atafurahi,
atanibariki.
Wakati wa Bunge la bajeti
wanaharakati wa haki za wanawake na Watoto waliwahamasisha Wabunge
watushughulikie Kwa ajili ya suala hili. Wakawa-pump wabunge data kuwa kwa siku
magnitude ya vifo vinavyotokana na sababu za uzazi ni sawa na 'coaster' moja
ipate ajali na iue watu wote! Wabunge waligeuka mbogo. Japokuwa namba hizi
zilikuwa exaggerated (zilizidishwa), walifikisha point kwetu. Kwamba lazima
tufanye kitu tofauti kwenye eneo hili. Mimi naanza kuchukua hatua. Vifo
vitokanavyo na uzazi havikubaliki!
Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB.,
NW-AMJW.
August 18th, 2016.

No comments:
Post a Comment