
MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara
imeamuru Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi afike
mahakamani kujieleza kwa nini asifungwe gerezani kwa kushindwa kutekeleza
hukumu inayohusu malipo ya Sh bilioni 1.2.
Mengi anatakiwa kufika mahakamani
hapo Agosti 24, mwaka huu kujieleza kutokana na kushindwa kutekeleza hukumu
iliyomtaka kuwalipa wafanyabiashara watatu, Muganyizi Lutagwaba, Eric Mshauri
na Charles Mgweo, Sh bilioni 1.2.
Alitakiwa kuwalipa fedha hizo
kutokana na mgogoro wa malipo ya uuzwaji wa hisa katika Kampuni ya Douglas Lake
Minerals Ltd ambayo kwa sasa inaitwa Handeni Gold Inc.
Kwa mujibu wa hati ya wito wa
kufika mahakamani, Mengi anatakiwa kufika mahakamani hapo Agosti 24, mwaka huu
ili ajieleze kwa nini asifungwe gerezani kama mfungwa wa madai kama sehemu ya
kukazia hukumu hiyo.
Mahakama imetoa hati hiyo kutokana
na wafanyabiashara hao kuwasilisha maombi katika hatua ya kukazia hukumu
iliyotolewa Januari 28, mwaka huu na Jaji Agathon Nchimbi wa mahakama hiyo.
Katika hati ya kiapo ya
wafanyabiashara hao, inadaiwa walifungua kesi dhidi ya Mengi na Kampuni ya K.M.
Prospecting Limited, wakidai malipo yaliyokuwa yamebakia ya dola 428,750,
100,000 na 70,000, kwa kila mmoja.

No comments:
Post a Comment