Kocha wa timu ya taifa ya Amavubi, Rwanda imemtimua kazi kocha wao
Mwingereza Jonathan McKinstry kwa matokeo yasiyo ya kuridhisha.
Taarifa hiyo ilitolewa na wizara ya michezo ya Rwanda
imethibitisha kuonyeshwa mlango kwa mkufunzi huyo.
Katibu mkuu wa wizara hiyo kanali Patrice Rugambwa
amesema sababu ya kumfuta kazi kocha huyo ni matokeo yasiyo ya kuridhisha ya
timu ya taifa Amavubi.
Rwanda kwa sasa ni ya tatu katika kundi lake kuwania
tiketi ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Afrika la mataifa nchini Gabon
mwakani ikiwa na alama 6.
Jonathan McKinstry alipewa mkataba wa kuifundisha
Amavubi mwaka jana na ukarefushwa mwaka huu baada ya kuiwezesha kucheza robo
fainali ya mashindano ya CHAN ilipoondolewa na DRC.
Timu hiyo kwasasa ipo katika nafasi 121 kwa ubora wa
FIFA.

No comments:
Post a Comment