Baada ya kufanya Mziki wa ndani Muda mrefu Dully atamani kutoka kimataifa - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 26 August 2016

Baada ya kufanya Mziki wa ndani Muda mrefu Dully atamani kutoka kimataifa

dully-12
Msanii mkongwe wa muziki wa bongofleva, Dully Sykes baada ya kufanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Inde’ amesema kilichobaki kwenye muziki wake ni kufungua milango ya kwenda kimataifa.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Dullly amesema kufanya vizuri nyumbani kutamsaidia kutoboa zaidi kimataifa kwa kuwa mashabiki wa nyumbani ndio wenye nguvu ya kumpush kwenda kimataifa zaidi.
“Kwa sasa plan yangu ni kwenda kifataifa, tayari nimeshafanya kila kitu kwenye huu muziki,” alisema Dully Sykes “Ninamashabiki ambao kwa sasa ni wazee na wengine wameshakufa na bado naendelea kutengeneza wapya, kwa hiyo kwangu mimi vingi nimeshafanya hapa nyumbani, sasa nataka kwenda mbele zaidi,”
Aliongeza, “Unajua katika muziki mtaji wa kwenda kimataifa unaanzia nyumbani, lazima uwe na mashabiki wa kutosha ambao wataweza kusupport muziki wako, kama nyumbani huna mashabiki nani atakusupport kimataifa, kwa hiyo mimi kwangu naweza kusema safari imeiva,”

Video yake ya wimbo ‘Inde’ aliyomshirikisha Harmonize tayari imeshaanza kuchezwa katika vituo mbalimbali vya runinga vya kimataifa huku katika channel ya Youtube ikiwa na views zaidi na laki nane ndani ya wiki moja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here