Belle 9 amekana kusaini na WCB na kudai kuwa alienda kutembelea kwenye
ofisi zao kwakuwa Diamond ni msanii mkubwa Afrika na amefanikiwa kufika mbali
kimuziki.
“Diamond ni msanii mkubwa Afrika ila Watanzania tumekuwa
wagumu kulikubali hilo,” amekiambia kipindi cha E News cha EATV. Belle 9
aliongeza kuwa alienda WCB kwa ajili ya kuwatembelea na kufanya nao mazoezi kwa
sababu anamheshimu Babutale kwakuwa ndiye aliyemkutanisha na menejimenti yake
aliyonayo.
Katika hatua nyingine, muimbaji huyo amesema kuwa bado
ana mkataba na menejimenti yake hivyo hawezi kusaini mkataba kwingine labda
mpaka utakapomalizika. Na kuhusu WCB amesema anaweza akasaini nao endapo
wakikubaliana na mambo yakienda sawa.
Hata kwa Rich Mavoko ilikuwa ni sinemaa kama hii lakini
hatimaye alijiunga na familia ya Wasafi.

No comments:
Post a Comment