Mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda amefunguka kwa
kusema kuwa wazo la jina la wimbo huo alikuja nalo AliKiba.
Muimbaji huyo ambaye alikiri wimbo huo kumwimbia
aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Shilole, amekiambia kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz
cha EATV kuwa hakuwa na wazo la jina la wimbo huo mpaka AliKiba alivyozungumzia
‘Jike Shupa’ kwenye chorus na wimbo huo.
“AliKiba ndiyo kila kitu, yeye ndiye aliyetoa neno la
‘Jike Shupa’,” alisema Nuh. “Wimbo kanikuta nimeshaurekodi na nimeshafanya
chorus yangu, na sikutaka kuiachia nikaenda kumshirikisha AliKiba akaniambia
nyimbo imekamilika nitaingiza nini humu, na nyimbo nzuri nikamwambia no, kwa
sababu nimekaa kimya muda mrefu nahitaji utofauti kwa sababu sijawai kufanya
kolabo, basi akasema okey, tukaenda studio tukamute chorus yangu AliKiba
akaingiza yake, ambapo katika kuandika kwake akaimba neno ‘Jike Shupa’, kwa
hiyo tilte ya nyimbo Ali anahusika,”
Wimbo huo umefanya vizuri katika vituo mbalimbali vya
radio na kumtambulisha rasmi Nuh Mziwanda katika muziki wa bongofleva.
No comments:
Post a Comment