Baada ya vocalist,
Rich Mavoko kusaini WCB ya Diamond, huwenda msanii wa muziki wa R&B kutoka
Morogoro, Belle 9 na yeye akasaini ndani ya label hiyo.
Muimbaji
huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Bugger Movie Selfie’ ameonekana akifanya
mazoezi ya bendi ya Diamond katika ofisi za WCB.
Kwa
mujibu wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Belle pamoja na Diamond
wameonekana wakiimba wimbo ‘Mdogo Mdogo’ kwa pamoja huku wakicheza.
Hatua
hiyo imefufua matumaini mapya kwa mashabiki wa kumuziki kuona huweza WCB
ikamsaini msanii hiyo kama ilivyofanya kwa Rich Mavoko.
Kwa
sasa label ya WCB ina wasanii wanne, Harmonize, Rich Mavoko, Raymond aka
Rayvany pamoja Queen Darlin.

No comments:
Post a Comment