Wapiga kura nchini Zambia wameanza kufika katika vituo vya
kupigia kura kushiriki uchaguzi wa urais na wabunge.
Kumekuwa na ushindani mkali na kipindi cha kampeni kilikumbwa na
vurugu.
Hali
hiyo ilimpelekea The Rock kulalamika kwenye Instagram akiwashutumu baadhi ya
waigizaji wa kiume wa filamu hiyo kuwa wana mambo ya kimbwiga na baadaye
kufahamika madongo hayo yalimhusu Diesel.
Na
sasa tovuti ya Page Six imeeleza sababu za mafahari hao kuchemshana damu.
“Vin
Diesel na Dwayne Johnson wamekuwa wakikorofishana muda wote kwenye utengenezaji
wa ‘Fast 8,’” chanzo kimoja kiliiambia Page Six. “Vin ana sifa ya kuwa pasua
kichwa, huchelewa kufika, huwafanya watu wamngoje, husimamisha utengenezaji na
huwa hawaheshimu watu kwenye utengenezaji. Uvumilivu ulimshinda Dwayne.”
Chanzo
hicho kiliongeza, “walikuwa na mkutano wa kujaribu kuyamaliza Jumanne.
Jumatano, Diesel alimaliza kufanya scene yake ya mwisho na Johnson alidaiwa
kumaliza sehemu yake kwenye filamu hiyo baadaye.”
Diesel
pia ni producer wa filamu hiyo huku TMZ ikidai kuwa The Rock hakufurahishwa na
baadhi ya maamuzi aliyoyafanya wakiwa location.
Diesel
amekuwa na sifa ya usumbufu Hollywood. Chanzo kimoja kilichowahi kufanya naye
kazi kimedai: Alikuwa akichelewa muda wote, alikuwa akifanya mambo kama
mwanamke na aliwahi kuchelewesha utengenezaji kabla, hivyo sishangai kuwa ndiye
ambaye The Rock amemchana.”
Lakini
vyanzo vingine vimedai kuwa ni The Rock ndiye amekuwa akichelewa kwenye
utengenezaji wa filamu hiyo kiasi cha kumtibua Diesel.
Kwenye Instagram, The Rock aliandika: My
female co-stars are always amazing… My male co-stars however are a different
story. Some conduct themselves as stand up men and true professionals… The ones
that don’t are too chicken s–t to do anything about it anyway. Candy asses.”

No comments:
Post a Comment