Kumekuwa na ushindani mkali na
kipindi cha kampeni kilikumbwa na vurugu.
Ushindani mkubwa unatarajiwa kuwa
kati ya Rais Edgar Lungu wa chama cha PF na mgombea wa upinzani wa chama cha
UPND Hakainde Hichilema.
Kuna jumla ya wapiga kura 6.7
milioni waliojiandikisha kupiga kura.
Kwa mara ya kwanza, mgombea urais
anatakiwa kupata asilimia 50 ya kura zitakazopigwa pamoja na kura moja zaidi
ili kuepusha awamu ya pili ya uchaguzi.
Bw Lungu alishinda uchaguzi mkuu
uliopita kwa kupata 48% ya kura.
Waangalizi wa uchaguzi huo wanasema
suala ya kudorora kwa uchumi litakuwa muhimu katika uamuzi wa wapiga kura.
Kuporomoka kwa bei ya shaba
nyekundi, tegemeo kuu la uchumi wa taifa hilo, kumesababisha kufungwa kwa
migodi na maelfu ya watu kupoteza kazi.
Ukuaji wa uchumi umepungua kwa nusu
na serikali ya nchi hiyo iliomba usaidizi wa kifedha kutoka kwa Shirika la
Fedha Duniani (IMF).
Isitoshe, sawa na nchi nyingine za
kusini mwa Afrika, Zambia imekumbwa na ukame mbaya zaidi katika kipindi cha
miaka 35.
Edgar Lungu alishinda uchaguzi
uliofanyika kufuatia kifo cha rais Michael Sata
Chama cha UPND (United Party for
National Development) kimemtuhumu Rais Lungu kwa kusimamia
"kusambaratika" kwa uchumi.
Lakini chama tawala cha PF (Patriotic Front) kinasema
kina mpango wa kutafuta njia mbadala za kukwamua uchumi.
Shirika moja lilionya kwamba ghasia
ambazo zimeshuhudiwa baina ya makundi pinzani ya kisiasa wiki za hivi karibuni
huenda zikawafanya baadhi ya watu kutojitokeza kupiga kura.
Shirika hilo la Zambian Elections
Information Centre linasema wahusika wamekuwa pia hawatii amri ya maafisa wa
usalama.
Hakainde Hichelema ameahidi
kusimamia vyema uchumi iwapo atashinda.
Jumanne, mkuu wa tume ya uchaguzi
Esau Chulu, aliwahimiza wagombea wawili wakoo kutochochea uhasama.
Upigaji kura utamalizika saa 18:00
saa za huko (16:00 GMT) na matokeo yanatarajiwa baadaye Ijumaa au Jumamosi.

No comments:
Post a Comment