Bosi wa lebo ya Bad
Boy, Diddy amehudhuria kwenye ziara ya Summer Sixteen ya Drake iliyofanyika
mjini Greensboro ikiwa ni siku chache baada ya kumaliza bifu lao.
Wawili
hao waliingia kwenye bifu hilo mwaka 2014 sababu ikiwa ni umiliki wa wimbo wa
‘0 to 100 / The Catch Up’ huku Diddy akiamini kuwa Drake amemuibia wimbo wake
huo.
Ugomvi huo uliwapa maneno ya kuongea wasanii wawili wenye bifu
na Drake akiwemo Meek Mill na Joe Budden kila mmoja akitumia nafasi hiyo mchana
kwenye wimbo wake. “Puffy almost caught a domestic when he smacked that bitch,”
alirap Meek Mill kwenye wimbo wake wa ‘Wanna Know’.
Hata hivyo mwaka uliofuata Drake alionekana kulimaliza bifu hilo
lakini Diddy alionekana kukaa kimya kwa muda wote bila kujibu lolote, kwa
mujibu wa TMZ inadaiwa kuwa wasanii hao wamemaliza matatizo yao kwa maongezi
yaliyofanyika kwa njia ya simu na hatimaye Diddy akahudhuria kwenye tamasha
hilo la Drek

No comments:
Post a Comment