Kiungo wa Manchester United, Mjerumani Bastian Schweinsteiger, ambaye
ameonekana kukosa nafasi kwa kocha Jose Mourinho, amesema hafikirii kujiunga na
timu nyingine ya barani Ulaya, na badala yake ataenda kucheza soka katika Ligi
ya Marekani au Asia.
Schweinsteiger alitumia account yake ya instagram kutoa taarifa kwamba
Manchester United ndio itakuwa klabu yake ya mwisho kuitumikia barani ulaya,
akisisitiza United ndio klabu pekee ambayo ingeweza kumuondoa Allianz Arena.
Hivyo kwa sasa ataendelea kubaki Manchester na kocha atakapomhitaji basi
ataenda kuitumikia klabu.

No comments:
Post a Comment